KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Saturday, March 6, 2010

Nigeria inaweza kushinda kombe la dunia


Kocha mpya wa Timu ya taifa ya Nigeria, Lars Lagerback ana imani kuwa timu ya Super Eagles wana vipaji vya kuiwezesha kufikia hatua za nusu fainali kwenye kombe la dunia huko Afrika ya kusini.
Kocha huyo ambaye ni raia wa Sweden alishuhudia Timu yenye wachezaji wasiocheza nje ya Nigeria wakiizaba Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo mabao 5-2 mjini Abuja mnamo siku ya jumatano.

Baada ya mechi hiyo kocha huyo aliulizwa kuhusu matarajio yake ya uwezekano wa kufuzu kucheza nusu fainali. Alisema kuwa kuna uwezekano mkubwa, nadhani kwamba kila kocha, kila taifa linaloingia mashindano yoyote huwa na matumaini ya ushindi.

Kocha huyo aliongezea kuwa Nigeria ina wachezaji wenye vipaji kwa hiyo wana kila fursa ya kupiga hatua kwenye mashindano ya kombe la dunia. Lakini aliongezea kuwa ni muhimu kufanya mipango ya kina ili Nigeria iweze kufanikiwa tukianza na kuwakusanya wachezaji wote katika kambi moja.

No comments:

Post a Comment