KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, March 6, 2010

Michael Owen nje kwa msimu mzima


Michael Owen nje kwa msimu mzima

Mshambulizi wa klabu ya soka ya Manchester United ya Uingereza, Michael Owen, akiwa na matatizo ya misuli ya paja, tangu mechi ya ushindi wa magoli 2-1 ya Kombe la Carling dhidi ya Aston Villa, hataweza kucheza tena msimu huu.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30, alifunga bao la kusawazisha katika mechi hiyo ya Wembley, lakini alipatwa na matatizo ya misuli alipokuwa akiukimbilia mpira katika kipindi cha kwanza. Kujeruhiwa kwa Owen kumempotezea matumaini yote ya kushirikishwa katika timu ya England.

Meneja wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, amesema kwamba kinyume na walivyofikiria hapo awali, hali ya Owen ni mbaya zaidi, na kwa kiasi fulani, alisema huenda hayo yalitokana na uwanja wa Wembley. Owen, ambaye ana mwaka mmoja uliosalia katika mkataba wake wa miaka miwili na Man U, awali alitazamiwa kupumzika kwa wiki chache tu. Atafanyiwa upasuaji Jumatatu.

No comments:

Post a Comment