KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, March 3, 2010

Balozi wa Rwanda nchini India, Lt. Jenerali. Kayumba Nyamwasa, ameng'atuka katika nafasi yake na kuvuliwa wadhifa huo na serikali ya Rwanda


Rwanda yamfuta balozi wake wa India

Balozi wa Rwanda nchini India, Lt. Jenerali. Kayumba Nyamwasa, ameng'atuka katika nafasi yake na kuvuliwa wadhifa huo na serikali ya Rwanda.
Jenerali Nyamwasa, ambaye ni kamanda wa zamani wa kundi la waasi nchini Rwanda lililotwaa madaraka mwaka wa 1994, anaarifiwa kuwasili nchini Uganda.

Serikali ya Rwanda imesema kamanda huyo wa zamani alihojiwa na maafisa wa upepelezi wa makosa ya jinai baada ya kurejea mjini Kigali kwa mashauriano.

Serikali ya Rwanda sasa inataka afisa huyo arejeshwe kutoka Uganda.

Jenerali Nyamwasa ni mwanadiplomasia wa pili wa Rwanda kuachia ngazi katika majuma ya hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment