KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, March 6, 2010

Polisi nchini Rwanda wanasema kumekuwa na milipuko miwili ya makombora katika mji mkuu wa Kigali


Milipuko ya makombora Kigali

Polisi nchini Rwanda wanasema kumekuwa na milipuko miwili ya makombora katika mji mkuu wa Kigali. Moja ya milipuko hiyo ilitokea karibu sana na eneo la makumbusho ya mauaji ya kimbari ya mwaka wa 94.
Hadi sasa hakuna mtu aliyeripotiwa kuuawa japo watu 16 walijeruhiwa.
Polisi wanasema bado wanachunguza mashambulizi hayo na hawajabaini waliohusika.

Mtu mmoja aliuawa katika mlipuko kama huo mwezi uliopita. Serikali ya Rwanda inalaumu waliokuwa maafisa wake wawili kwa kupanga mashambulizo hayo ya mwezi jana.

Mmoja wa maafisa hao, Lt Jen Faustin Kayumba Nyamwasa, amekanusha madai hayo na amekimbilia Afrika Kusini. Bwana Kayumba ambaye alikuwa balozi wa Rwanda nchini Inidia, analaumu serikali ya Rais Paul Kagame kwa kupanga njama za kuzima wapinzani wake.

No comments:

Post a Comment