KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, March 3, 2010

Congo yatakiwa kumshitaki afisa wa kijeshi


Congo yatakiwa kumshitaki afisa wa kijeshi

Mashirika ya kutetea haki za binadamu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo yamewasilisha malalamiko serikalini dhidi ya afisa mwandamizi wa kijeshi katika jimbo la Kivu ya Kaskazini.
Mashirika hayo--likiwemo, Human Rights Watch--linawashtumu askari walio chini ya Col Innocent Zimurinda kwa mauaji ya watu wengi, ubakaji na kuwalazimisha watoto kutumika kama wapiganaji katika vita.

Katika taarifa waliyoitoa, mashirika hayo yanaitaka serikali imsimamishe kazi na kumfungulia mashtaka kamanda huyo.

Wito wa mashirika hayo umetolewa wakati serikali ya Congo ikijiandaa kutekeleza mashambulizi makubwa dhidi ya waasi,ambayo yanaungwa mkono na Umoja wa Mataifa.

Mashirika ya kutetea haki za binadamu yanahofia kuwa raia hawatolindwa katika operesheni hiyo ikiwa Col Zimurinda atashirikishwa.

Kamanda huyo hakuweza kupatikana ili kujibu shutma hizo.

No comments:

Post a Comment