KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, February 6, 2010

Yar'Adua wa Nigeria kukabidhi madaraka?Mshauri wa Rais wa Nigeria ameiambia BBC, Bw Umaru Yar'Adua anayeugua ataandika barua kukabidhi madaraka kwa makamu wake.
Barua hiyo, itayomwarifu rasmi seneta kwamba Bw Yar'Adua yuko katika likizo ya matibabu, inamaanisha moja kwa moja kuwa makamu wake atakaimu nyadhifa ya urais.Awali washirika wake walipinga wito wa Rais Yar'Adua kukaa kando.

Amekuwa akipata matibabu hospitalini nchini Saudi Arabia tangu mwezi Novemba, na kuzua wasiwasi wa kuwepo na ombwe katika madaraka na maanadmano mitaani.

Rais Yar'Adua ana matatizo ya moyo na amekuwa na matatizo ya figo kwa muda mrefu.

No comments:

Post a Comment