KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Saturday, February 6, 2010

Mswada kuchunguzwa upya Uganda


Naibu waziri wa mambo ya nje wa Uganda Okello Oryem, amesema Waganda wanachunguza shutuma zilizotolewa kote duniani, kuhusu mswada unaopendekeza hukumu ya kifo kwa watu watakao patikana kuwa wapenzi wa jinsia moja.
Bwana Oryem ameiambia BBC kuwa mswada utakaowasilishwa bungeni, utakuwa tofauti na ule wa awali. Matamshi hayo yametolewa siku moja tu baada ya rais wa Marekani Barack Obama, kusema mswada huo unapendekeza sheria za chuki.

Rais Obama alisema sio dhamira nzuri kuwalenga wapenzi wa jinsia moja kutokana na hali yao.

No comments:

Post a Comment