KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, February 6, 2010

Uchina yaikosoa ICC kuhusu rais wa Sudan
Uchina imesema hatua ya Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) ya kutaka kumwongezea makosa ya mauaji ya kimbari Rais wa Sudan, Omar Hassan al-Bashir, itaathiri juhudi za amani nchini Sudan.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Uchina, alisema hali nchini Sudan iko katika mahali pagumu, ukizingatia suala la Darfur na mpango wa amani kati ya Kaskazini na Kusini.

Siku ya Jumatano majaji wa mahakama ya rufaa waliamuru tathmini mpya ifanyike kuhusu uamuzi wa hapo awali juu ya hatua inayoagiza kukamatwa kwa Rais Bashir .

Katika hati iliyotolewa na mahakama hiyo mwaka uliopita, Rais Bashir alidaiwa kutenda uhalifu wa kivita katika jimbo la Darfur. lakini hati hiyo haikujumuisha mauaji ya kimbari.

Uchina ina uhusiano mkubwa wa kibiashara na Sudan.

No comments:

Post a Comment