KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Saturday, February 6, 2010

Waziri mkuu Kenya ataka Waziri ajiuzulu
Waziri mkuu wa Kenya Raila Odinga, amewataka waziri wa elimu na katibu wake kujiondoa kazini kutokana na kashfa ya ufisadi ambayo imekumba wizara hiyo.
Uchunguzi uliofanywa katika wizara hiyo hivi majuzi umedhihirisha kuwa zaidi ya dola milioni 1 za kufadhili mpango wa elimu ya msingi zimefujwa.

Kauli ya waziri mkuu imetolewa katika mkutano wa maafisa wakuu serikalini ulioitishwa na Rais wa nchi hiyo Mwai Kibaki ili kujadili suala la ufisadi.

Bwana Odinga amesema sharti maafisa wakuu serikalini wawajibike ili kuongoza vita dhidi ya ufisadi.

Amependekeza kuwa Rais amuulize waziri wa elimu Profesa Sam Ongeri na Katibu wake Karega Mutahi wajiondoe kazini.

Serikali za Uingereza na Marekani tayari zimesitisha ufadhili wao wa elimu kwa serikali ya Kenya, kutokana na sakata hiyo.

No comments:

Post a Comment