KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, February 4, 2010

Soyinka ashutumu uamuzi wa Marekani

Mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel, mwandishi maarufu wa Nigeria, Wole Soyinka, amesema Marekani, inapaswa kuorodhesha Uingereza katika orodha ya mataifa yaliyowekewa tahadhari ya kigaidi kama vile ilivyoiweka Nigeria.
Soyinka ameyasema hayo mwezi mmoja, baada ya raia mmoja wa Nigeria aliyesomea uingereza, kujaribu kujilipua ndani ya ndege mjini Detroit, nchini Marekani, mkesha wa siku kuu ya Krismasi.

Bwana Soyinka, amesema Uingereza, ni kitovu cha Waislamu wenye msimamo mkali. Amesema mshukiwa huyo raia wa Nigeria, aliyejaribu kujilupua, alianza kuwa na msimamo mkali wakati alipokuwa akiishi nchini Uingereza, na wala sio Nigeria

No comments:

Post a Comment