KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Thursday, February 4, 2010

Rais Idriss Deby Kuzuru Sudan wiki ijayo

Rais wa chad, Idriss Deby, ametangaza kuwa atazuru mji mkuu wa Sudan, Khartoum, jumatatu ijayo, kufanya mashauriano na rais wa nchi hiyo Omar Al Bashir.
Serikali ya Chad na Sudan, zimetia saini mikataba kadhaa iliolenga kusitisha uhasama kati yao, lakini harakati za waasi katika pande zote mbili zimekuwa zikichochea uhasama kati ya nchi hizo mbili.

Rais Deby, ambaye hujiamini kuwa mtu wa majadaliano, anasema vita haviwezi kutatua mzozo wa aina yoyote. Rais huyo alizuru Sudan mara ya mwisho mwaka wa 2004.

No comments:

Post a Comment