KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Thursday, February 4, 2010

Rais wa Nigeria atakiwa kung'oka

Kundi la wakuu wa vyombo vya habari limeonya kuwa Rais wa Nigeria anayeugua Umaru Yar'Adua lazima akabidhi madaraka kwa makamu wake katika kipindi cha siku saba au ajiuzulu.
Wamiliki wa magazeti 17 na mashirika ya vyombo vya habari wamesema katika ujumbe wa pamoja kuwa Bw Yar'Adua lazima watamshitaki kwa kutumia madaraka vibaya kama atashindwa kutekeleza matakwa yao.

Rais huyo anayeugua amekuwa katika hospitali moja ya Saudi Arabia tangu mwezi Novemba.

Kumekuwa na kesi kadhaa za kisheria zikihoji uwezo wa Rais kuongoza nchi akiwa amelazwa.

Katika kesi ya mwisho, mahakama kuu imesema hakukuwa na kipengele chochote cha kikatiba kwa kiongozi yeyote wa mpito kuteuliwa

No comments:

Post a Comment