KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, February 9, 2010

Jimmy Carter awasili nchini Sudan




Aliyekuwa rais wa Marekani Jimmy Carter amewasili nchini Sudan kwa mashauriano na rais wa nchi hiyo, Omar al-Bashir na maafisa wengine wakuu serikalini.
Carter anatarajiwa kuelezea wasi wasi wake kuhusu uchaguzi mkuu nchini humo unaopangwa kufanywa mwezi Aprili.

Bwana Carter pia anatarajiwa kushauriana na maafisa wa tume ya uchaguzi nchini humo. Mapema mwaka huu Bw. Carter alisema tume hiyo inakabiliwa na matatizo ya kifedha na haiungwi mkono ipasavyo na serikali ya nchi hiyo.

Ameelezea kusikitishwa kwake na kile anachosema ni usajili wa idadi ndogo ya wapiga kura na mapigano yanayoendelea katika eneo la darfur.

Wakfu wake, The Carter Center kwa sasa unatoa mafunzo kwa maafisa 3,000 watakaochunguza jinsi uchaguzi huo utakavyoendeshwa.

No comments:

Post a Comment