KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, January 18, 2010

Waathiriwa Haiti wapata Afueni
Waathiriwa Haiti wapata Afueni

Hatimaye msaada umeanza kuwafikia baadhi ya waathiriwa wa tetemeko la ardhi lililotokea Jumanne katika mji mkuu wa Haiti, Port-au-Prince, huku wafanyakazi wa kutoa misaada wakianza kusambaza maji na chakula.

Wanaondesha shughuli hiyo ni wafanyakazi kutoka Marekani wakishirikiana na wanajeshi wa nchi hiyo.

Hata hivyo, upungufu wa misaada hiyo ndiyo umekuwa changamoto kubwa kwa waathiriwa walio katika hali mbaya zaidi.

Mwandishi wa BBC mjini humo amesema wamesalia tu kusikia vilio vya watu wakitaka chakula na maji.

Balozi wa Haiti katika umoja wa Mataifa, Raymond Joseph, ameifahamisha BBC kuwa athari za mtetemeko zimeonyesha mfumo wa miundo mbinu duni katika mji wa Port-au-Prince.No comments:

Post a Comment