KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Sunday, January 10, 2010

MAISHA YA MZEE KAWAWA NI ELIMU BORA KATIKA ULIMWENGU WA SIASA.


SIFA ZA MZEE KAWAWA:
“ ALIKUWA MTU JASIRI, MUADILIFU, ASIYEKUWA NA MAKUU, ASIYEKUWA NA TAMAA, MCHAPAKAZI, MVUMILIVU, HAKUWA MTU WA KUJIKWEZA ANAYEABUDU UBWANA MKUBWA, KABISA HAKUWA MVIVU, MWENYE HEKIMA, BUSARA, ANAYEJALI KILA MTU, HAKUOGOPA LAWAMA”
• HIZO NI BAADHI YA SIFA ZILIZO MIMINWA NA VIONGOZI WA NGAZI MBALIMBALI ZA CHAMA NA SERIKALI KWA MAREHEM MZEE RASHID MFAUME KAWAWA KUFUATIA KIFO CHAKE DECEMBER 31.


• PROF. LIPUMBA ALIWASILSHA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUPITIA VYAMA VYA SIASA, PROF. LIPUMBA, ALISABABISHA WAOMBOLEZAJI KUSAHAU KWAMBA WAKO MSIBANI NAKUJIKUTA WAKIMPIGIA MAKOFI MARA ALIPOHITIMISHA SALAMU ZAKE, HUKU RAIS JAKAYA KIKWETE, AKIONGOZA JUKWAA LA VIONGOZI WAKUU WA SERIKALI KUSIMAMA NA KUMPA MKONO.
• PROF. LIPUMBA KATIKA SALAMU ZAKE, ALISEMA PAMOJA NA KUWA MZEE RASHIDI KAWAWA, KUWA CCM KINDAKINDAKI, LAKINI HAKUWAHI KUVIBEZA VYAMA VIPYA VYA SIASA VILIVYOANZISHWA.

• PROF. LIPUMBA, ALIMUELEZEA MZEE KAWAWA, WAKATI HUO AKIWA MAKAMU MWENYEKITI WA CCM, KUWA NI MIONGONI MWA VIONGOZI WACHACHE AMBAO NYAKATI ZA SIASA ZILIPOBADILIKA NA KUINGIA KATIKA MFUMO WA VYAMA VINGI VYA SIASA, ALIKUWA NA MSTARI WA MBELE KUUNGA MKONO HOJA HIYO. ALISEMA, HAYATI MZEE KAWAWA, KATIKA UHAI WAKE WOTE TAIFA LIKIWA NDANI YA VMFUMO WA VYAMA VINGI VYA SIASA ALIHUZUNISHWA NA WANASIASA WANAOHAMAHAMA VYAMA KWA KUKIMBILIA NYADHIFA AU KUGANGA NJAA KATIKA VYAMA VINGINE.
• “WATANZANIA NA HASWA VIONGOZI WA KISIASA TUNAWAJIBIKA KUMUENZI SIMBA WA VITA, KWA KUFUATA MFANO WA UADILIAFU WAKE KATIKA UONGOZI WA KISIASA, SIASA SI BIASHARA YA KUJILIMBIKIZIA MALI BALI NI DHIMA YA KUUTUMIKIA UMMA KWA UADILIFU. WANAOTAKA MALI MILANGO YA BIASHARA NA UJASILIAMALI IKO WAZI WAENDE HUKO, NA SI KATIKA SIASA.
• “SIASA WAACHIE WALE WALIOTAYARI KUUTUMIKIA UMMA BILA MAKUU KAMA ALIVYOFANYA MAREHEMU MZEE RASHIDI KAWAWA, WALA MAREHEMU (KAWAWA) HAKUPENDA WANASIASA WA AINA YA KUGANGA NJAA, KWA KUHAMAHAMA VYAMA.” ALISEMA PROF. LIPUMBA, KATIKA SALAMU ZAKE HIZO NA KUJIKUTA AKIPIGIWA MAKOFI NA WAOMBOLEZI.
• MANENO YA MUFTI, SHEIKH SHAABA BIN SIMBA
“YANATOSHA MAUTI KUWA WAADHI” KILA MMOJA WETU SASA KATIKA MOYO WAKE ANAZUNGUMZIA KIFO CHA MZEE WETU RASHIDI MFAUME KAWAWA, INNALILLAH WAINNAILLAHIR RAJIUUN.
MUFTI SIMBA ALIYASEMA HAYO MUDA MCHACHE KABLA YA KUONGOZA IBAADA YA SWALA YA JENEZA KUMSWALIA ALIYEKUWA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS HAYATI MZEE RASHID MFAUME KAWAWA, NYUMBANI KWAKE MADALE, NJE KIDOGO YA JIJI LA DAR ES SALAAM, MAPEMA JUMAMOSI ILIO

No comments:

Post a Comment