KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, January 18, 2010

Mwanamke kugombea urais Rwanda
Siasa zimeanza kunoga katika eneo la maziwa makuu ambapo Rwanda inajiandaa kwa uchaguzi wake mkuu mwezi Agosti mwaka huu.
Kiongozi wa chama cha upinzani cha United Democratic Forces (FDU), Bi Ingabire Victorie amerejea nchini baada ya miaka 16 ukimbizini nchini Uholanzi.

Bi Ingabire amerejea na nia ya kugombea kiti cha Urais katika uchaguzi utakaofanyika mwezi Agosti.

kwa mujibu wa Bi Ingabire, nia yake ni kuondoa hali ya uoga miongoni mwa wananchi wa Rwanda na kuleta demokrasia ambayo kwa mtazamo wake haipo nchini humo.

No comments:

Post a Comment