KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, January 18, 2010

Maafisa wamesema polisi Kenya wamewakamata wabunge 16 wa kisomali na maafisa wengine wa serikali katika kuwasaka wahamiaji wanaoishi kinyume na sheria


Wabunge wa Kisomali wakamatwa Kenya

Maafisa wamesema polisi Kenya wamewakamata wabunge 16 wa kisomali na maafisa wengine wa serikali katika kuwasaka wahamiaji wanaoishi kinyume na sheria mjini Nairobi.
Takriban watu 300 walikamatwa katika uvamizi huo wa polisi mjini Eastleigh, eneo linalokaliwa zaidi na watu wa asili ya kisomali.

Kiongozi maarufu wa kiislamu kutoka Kenya Al-Amin Kimathi naye pia amekamatwa.

Msako huo wa polisi umefanywa kufuatia ghasia zilizotokea Ijumaa baina ya polisi na makundi yanayopinga mpango wa kumwondosha Sheikh Abdullah al-Faisal.
Waziri wa mambo ya ndani wa Kenya George Saitoti amelishutumu kundi la wapiganaji la kiislamu la al-Shabab akiwahusisha na ghasia hizo, lililosababisha vifo vya takriban watu watano.

Lakini msemaji wa al-Shabab amekana kuhusika na ghasia hizo

No comments:

Post a Comment