KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, January 18, 2010

MIMBA NDIO MSINGI WA HIFADHI YA MTOTO MAISHANI.


MIMBA NDIO MSINGI WA HIFADHI YA MTOTO MAISHANI.
MIMBA NI KIFAA KINACHOHIFADHI MTOTO KATIKA TUMBO LA MWANAMKE. MWANAMKE ANAPOKUWA NA MBIMBA HUITWA MJAMZITO.
UPATIKANAJI WA MIMBA MAISHANI
MIMBA INAPATIKANA, KUPITIA NJIA YA JINSIA MBILI MAISHANI.
JINSIA HIZO LAZIMA ZIWE YA KIUME NAYA KIKE. KATIKA MFUMO WA KUZALIANA KWA VIUMBE (BINADAMU, WANYAMA, NDEGE, MIMEA, WADUDU, SAMAKI….N.K, MWENYEZI MUNGU ALIUMBA AINA MBILI ZA JINSIA KATIKA KILA KIUMBE (BINADAMU, WANYAMA, NDEGE, WADUDU…..N.K) ILI VIWEZE (VIUMBE) KUISHI KATIKA MAISHA YA KUZALIANA MAISHANI.
MTAZAMO WETU WAKUZALIANA KWA LEO UNAHUSU UMBO LA BINADAMU. KATIKA BINADAMU KUNA JINSIA MBILI AMBAZO NI JINSIA YA KIUME NAYA KIKE.


ILI MWANAMKE AWEZE KUPATA MIMBA, LAZIMA AWE NA UHUSIANO NA WATENDO LA NDOA NA JINSIA YA KIUME. UHUSIANO WA KIJINSIA UTASABABISHA KUPANDA MBEGU YA MWANAMME KATIKA SHAMBA LA MWANAMKE. MBEGU YA MWANAMME IKIKUTANA NA YAYI LA MWANAMKE, KITAKACHOTOKEA NDANI YA TUMBO LA MWANAMKE NI MIMBA AU UJAUZITO.
MUDA WA MIMBA YA BINAADAMU
KILA KIUMBE MWENYEZI MUNGU ALIKIKADILIA MUDA WAKE WAKUISHI KATIKA TUMBO LA MAMAAKE NA MUDA WA KUISHI KATIKA UHAI WA KUJITEGEMEA NA MUDA WA KIFO (MWISHO WA MAISHA YA DUNIA) CHAKE MAISHANI.
TUKIJA KATIKA MTAZAMO WA UMBO LA BINADAMU, TUTAMKUTA BINADAMU ANAISHI KATIKAMFUMO WA MUDA WA MIEZI TISA (9 MONTH) TUMBONI MWA MAMAAKE.
MIEZI TISA NI SAWA NA WIKI 36(36 WKS)
AU SAWA NA SIKU 252 (252 DAYS) AU MASAA 6,048 (6,048 HRS) AU DAKIKA 362,880
(362,880 MINUTES) AU SEKUNDE 21, 772,800 (21, 772,800 SECONDS).


UVUMILIVU WA MJAMZITO MAISHANI
MWANAMKE MJAMZITO, HUISHI KATIKA HALINGUMU ANAPOKUWA NA MIMBA. MIMBA INABADILISHA HALI YA MAISHA YA MWILI NA ROHO VYA MWANAMKE HUSIKA. KUMBUKA YA KWAMBA ROHO NA MWILI NDIVYO VYENYE KUUNDA KIFAA KINACHOITWA NAFSI YA KIUMBE HASA MWANADAMU.
MIMBA INAMFANYA MWANAMKE MJAMZITO KUJIHISI KUCHOKA NA MARANYINGINE KUWA NA HASIRA ZA GHAFLA AU MARANYINGINE KUISHI KATIKA MFUMO WA KUHISI KICHEFUCHEFU. MIMBA INAWEZA KUMFANYA MWANAMKE MJA MZITO KUCHUKIA MMEWE AU KUMPENDA MMEWE ZAIDI. NA MARANYINGINE KUNA AINA YA MIMBA AMBAYO INAMFANYA MWANAMKE MJAMZITO KUISHI KATIKA MAZINGIRA YA KUTOJIJALI KIUSAFI.
UVUMILIVU WA MWANAMKE MJAMZITO NI WAHALI YA JUU KABISA. WAKINA MAMA WAJAWAZITO MARANYINGI HUKOSA HAMU YA KULA. KUNA BAADHI YA WANAWAKE WAJAWAZITO AMBAO HUTUMIA UDONGO KAMA KIBURUDISHO CHA KUTAFUNA AU KULAMBA.
YOTE HAYA YANASABABISHWA NA MFUMO WA UJAUZITO WAKE (MWANAMKE).

UPENDO :
MWANAMKE MJAMZITO ANAHITAJI MAPENZI YA HALI YA JUU KABISA, KUTOKA KWA MME WAKE KISHA KATIKA WATU WALIOMZUNGUUKA.
LAZIMA MWANAMME (MHUSIKA WA MIMBA) ATAMBUE KWAMBA MKE WAKE YUPO KATIKA MABADILIKO YA KIMWILI NA KIROHO (NAFSI). IKIWA MME WAKE ATALITAMBUA HILI MAPEMA, ATAJIKUTA AKIISHI NA MKEWAKE (MJAMZITO) KATIKA HALI YENYE AMANI NA UTULIVU.
MWANAMKE MJA MZITO ANAHITAJI CHAKULA CHA KUTOSHA NA KUNYWA MAJI YA KUTOSHA. MWANAMKE MJAMZITO ANAHITAJI MUDA WA KUPUMZIKA.
SHIDA YA MWANAMKE MJAMZITO :
SHIDA YA MWANAMKE MJAMZITO NI KUKIMBIWA NA MMEWAKE. MWANAMKE ANAPOISHI KATIKA MAZINGIRA YA KUBEBA MIMBA YENYE UPUNGUFU WA UKARIBU WA MME, HII NI HATARI JUU YA MBEBAJI MZIGO (MWANAMKE MJAMZITO). KITENDO HICHO KITAONGEZA MAUMIVU NDANI YA NAFSI YA MWANAMKE MJAMZITO. MIMBA NI KIFAA CHE MUUNGANO WA MBEGU YA MME NA YAYI LA MWANAMKE. MIMBA INAHITAJI ULINZI WA PANDE ZOTE MBILI (MKE NA MME) LICHA YA KUWA INABEBWA NA MTU MMOJA (MKE). MWANAMME ANAHITAJI KUBEBA MZIGO WA MIMBA YA MKEWE KIROHO (KUISHI KATIKA HISIA YA HURUMA JUU YA UJAUZITO WA MKEWE) KITENDO HICHO KITAMFANYA MWANAMME NA MWANAMKE WAISHI KATIKA MAZINGIRA YA KUHURUMIANA NA KUVUMILIANA MAISHANI.
UTATA WA MIMBA :
UTATA WA MIMBA UNAWEZA KUJITOKEZA PALE AMBAPO MWANAMME ATAIKATAA. MARANYINGI JAMBO HILO LINAJITOKEZA PALE AMBAPO MWANAMKE NA MWANAUME WANAPOISHI BILA YA NDOA. TENDO LA NDOA LENYE UKOSEFU WA MSINGI WA NDOA, MARANYINGI NDIO NJIA YA KUZALISHA WATOTO HARAMU AU WATOTO WASIOFAHAMU BABA ZAO MAISHANI. KUNA WATOTO AMBAO WANAZALIWA HADI KUFA BILA KUWATAMBUA BABA ZAO NA KUNAWATOTO WENGINE HUJIKUTA KATIKA MAZINGIRA YA KUISHI NA BABA ZAO WA KAMBO. NA MARANYINGINE UTAWAKUTA BAADHI YA WANAUME, AMBAO WANAMASHAKA JUU YA UHALALI WA WATOTO WA WAKE ZAO (WANAMASHAKA KWAMBA WATOTO SIO WA KWAO). MARANYINGI YOTE HAYO HUSABABISHWA NA UTATA WA MIMBA HUSIKA. MSINGI WA UTATA WA MIMBA UNATOKANA NA UPUNGUFU WA MAPENZI ULIOKO BAINA YA WALE WAHUSIKA WA MIMBA. MSINGI WA UPUNGUFU WA MAPENZI UNATOKANA NA UAMINIFU MDOGO BAINA YA MKE NA MME.

MAANDALIZI YA MIMBA:
KILA JAMBO MAISHANI LINAHITAJI MAANDALIZI. UKIANGALIA ASILIMIA KUBWA YA MIMBA HASA WALE WANAWAKE WENYE UJAUZITO WENYE MSINGI WA MAUMIVU YA MWILI NA KIROHO, UTAWAKUTA WENGI WAO WAMEBEBA MIMBA BILA KUJIPANGA AU WAUME ZAO KUJIPANGA MAISHANI.
MIMBA INAHITAJI MPANGILIO WA KIAFYA NA KIUCHUMI MAISHANI. UPUNGUFU WA KIMOJA UNAWEZA KUATHIRI MAZINGIRA YA MUUNGANO WA MIMBA (MKE NA MME) AU KUATHIRI MAISHA YA MTOTO. MTOTO ANAWEZA KUKUMBWA NA KIFO CHA KUTOLEWA TUMBONI KABLA YA WAKATI AU MTOTO ANAWEZA KUZALIWA KABLA YA WAKATI WAKE AU MTOTO ANAWEZA KUZALIWA NAKUISHI KATIKA MAZINGIRA YA KUTOMJUA BABA MZAZI AU MTOTO ANAWEZA KUJIKUTA AKIISHI KATIKA UPUNGUFU WA MAPENZI YA BABA. ATHARI ZOTE HIZO ZINASABABISHWA NA UPATIKANAJI WA MIMBA WENYE UPUNGUFU AU UKOSEFU WA MAANDALIZI MAISHANI.

SIRI YA MIMBA MAISHANI :
MIMBA NI MFUKO WENYE SIRI YA UMBO NA JINSIA MAISHANI. NIWAJIBU WA KILA BINADAMU KUKUBALI KWAMBA HAKUNA MTU MWENYE UWEZO WA KUJIPANGIA KUINGIZA MBEGU YA KIUME AU YA KIKE KATIKA MFUKO WA KIZAZI MAISHANI. MWENYEZI MUNGU NDIE MWENYE UJUZI WAKILICHOMO TUMBUNI (KATIKA MFUKO WA KIZAZI) AU MPANGILIO WA KIZAZI CHA WANANDOA HUSIKA.
KUNA BAADHI YA WATU WENYE KUPENDELEA KUZAA JINSIA FULANI (MTOTO WA KIUME AU WA KIKE) MAISHANI MWAO LAKINI WANASAHAU YA KWAMBA MUUMBA WAKILA KITU (MUNGU) NDIE MWENYE KUTOA MTOTO WA KIUME AU WAKIKE MAISHANI. WANANDOA WANAFURSA YA KUPELEKA MAOMBI YAO KWA
• UMBILE LA BINAADAMU NILENYE UKAMILIFU WA VIUMGO MAISHANI MWAKE. KAMA TUNAVYOSHUHUDIA AU KUSIKIA KATIKA VYOMBO VYA HABARI AU MIDOMONI MWA WATU, KUNA BAADHI YA BINADAMU AMBAO WANAZALIWA KATIKA HALI YA ULEMAVU WA MACHO, USIKIVU, HISIA, KUZUNGUMZA, KUTEMBEA, MIKONO, MIGUU, TUPU……..N.K, YOTE HAYO YANATOKANA NA MAPENZI YA MUNGU KATIKA KUUMBA KIUMBE HUSIKA. HAKUNA MTU MWENYE KUPENDA KUZAA MTU MLEMAVU, LAKINI JAMBO HILO HUJA KATIKA HALI YA MTIHANI MAISHANI. MTIHANI HUU UNAWEZA UKASABABISHA MGOGORO BAINA YA WANANDOA. MGOGORO WA WANANDOA KUHUSU ULEMAVU WA MTOTO HUSIKA UNAANZISHWA NA UPUNGUFU WA IMANI JUU YA MUNGU. MTU MWENYE UPUNGUFU WA IMANI JUU YA NAFASI YA MUNGU KATIKA KUUMBA, MARANYINGI HUWA NA UPINZANI JUU YA NEEMA NA REHEMA YA MUNGU MAISHANI MWAKE.
• IMANI NI KIFAA KINACHOMFANYA MTU KUAMINI JAMBO FULANI PASINA SHAKA NDANI YAKE. INAPOTOKEA MWANAMKE KUJIFUNGUA MTOTO WA KIUME, WAKIKE AU MLEMAVU WA AINA FULANI, NI WAJIBU WETU SISI BINADAMU KUKIPOKEA KIUMBE KILE KATIKA MFUMO WA AMANI NA UTULIVU. AMANI NA UTULIVU UTATOKANA NA KUMTAMBUA MWENYEZI MUNGU KWAMBA YEYE NDIE MUUMBAJI NA MTOAJI BORA MAISHANI.

No comments:

Post a Comment