KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Sunday, January 10, 2010

Guinea yasema kiongozi wa muda "si mgonjwa"
Waziri wa afya wa Guinea amekanusha taarifa kuwa kiongozi wa muda wa kijeshi nchini humo, Generali Sekouba Konate, amepelekwa Senegal kwa matibabu.
Bw Abdoulaye Cherif Diaby aliambia radio ya taifa kuwa Bw Konate anaenda mjini Dakar, kwa ziara rasmi, na wala si mgonjwa.

Hapo kabla, maafisa wa serikali ya Guinea ambao majina yao hayakutajwa walisema kuwa kiongozi huyo wa muda anaugua, na huenda anasumbuliwa na tatizo la ini.

Siku ya Ijumaa, shirika la habari la taifa la Senegal liliarifu kuwa serikali ya mjini Dakar inatuma ndege nchini Guinea kumchukua Generali Konate.

Bw Konate amekuwa akikaimu nafasi ya urais, wakati Capt Moussa Dadis Camara akiendelea kupata nafuu nchini Morocco, baada ya jaribio la kutaka kumwua mwezi December mwaka uliopita.

No comments:

Post a Comment