KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Sunday, January 10, 2010

Rais Gbagbo aishtumu tume ya uchaguzi
Rais wa Ivory Coast, Laurent Gbagbo, ameishtumu Tume Huru ya Uchaguzi kwa ufisadi, na kutumia vibaya mfumo wa uandikishaji wa wapiga kura.
Alisema vitendo hivyo vya tume vilisababisha kuahirishwa kwa uchaguzi kwa muda mrefu..

Rais Gbagbo alisema tume hiyo inajaribu kuwajumuisha maelfu ya wapiga kura ambao hawana haki ya kupiga kura.

Ivory Coast kwa muda mrefu imewavutia wahamiaji wengi kutoka nchi jirani, na suala la kuwapatia haki ya kupiga kura ndilo lilisababisha kuzuka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka wa 2002.

Kufuatia mapigano hayo imegawanyika kati ya kusini na kaskazini tangu wakati huo.

No comments:

Post a Comment