KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Sunday, January 10, 2010

'Aliyewaua maafisa wa CIA' aliapa kulipa kisasi
Picha ya video inayodaiwa kuwa ya raia wa Jordan aliyewaua maafisa wa marekani nchini Afghanistan inaonyesha mtu huyo akiapa kulipa kisasi.
Katika video iliyoonyeshwa na kituo cha televisheni cha al-Jazeera, inamuonyesha Khalil Abu-Mulal al-Balawi akiahidi kulipa kisasi kwa kifo cha kiongozi wa Taliban nchini Pakistan Baitullah Mehsud.

Anaonekana akiwa karibu na mrithi wa Mehsud, Hakimullah Mehsud,ingawa hakutambulishwa kwenye video hiyo.

Uhakika wa video hiyo haujathibitishwa.Watu wanane waliuawa kwenye shambulio hilo la bomu. Saba walikuwa maafisa wa ujasusi wa marekani na mmoja afisa wa ujasusi wa Jordan.

No comments:

Post a Comment