KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Sunday, January 10, 2010

Arsenal yabanwa na Everton 2-2
Kocha Arsene Wenger amesema ameridhika na sare ya magoli mawili dhidi ya Everton katika mechi ambayo Arsenal wangeweza kufungwa 2-3.
Mchezaji wa akiba Tomas Rosicky alifunga dakika za majeruhi kusawazisha pointi muhimu kwa Arsenal.

Leon Osman aliwapa wageni goli la kwanza dakika ya 12 alipomalizia kwa kichwa kona ya Landon Donovan.

Arsenal walijibu mapigo wakati mpira uliopigwa na ulipomgonga Tim Howard kabla ya kutinga wavuni.

Steven Pienaar aliwatoka walinzi wa Arsenal na kukimbia na mpira hatimaye kuudokoa juu ya mlinda mlango Manuel Almunia kuandika goli la pili, lakini Rosicky alitandika mkwaju ulioikoa Arsenal dakika ya 90+2.

Arsenal Wenger alikiri kuwa wachezaji wake walishindwa kucheza kama ilivyotakiwa.

No comments:

Post a Comment