KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Sunday, January 10, 2010

Birmingham yaikwamisha Manchester United

Manchester United ilishindwa kupanda kilele cha ligi kuu ya England baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na Birmingham City.
Mpira uliomshinda Jonny Evans kuuondosha katika eneo la hatari ulitoa fursa kwa Cameron Jerome kutikisa nyavu muda mfupi kabla ya mapumziko.

Goli la kujifunga mwenyewe la Scott Dann liliwafanya United kusawazisha, ingawa katika mazingira ya utata kutokana na mwamuzi Mark Clattenburg kutofautiana na msaidizi wake kuhusu uwezekano wa offside.

Matokeo hayo yanaiweka United pointi moja nyuma vinara Chelsea, ingawa wamecheza mechi moja zaidi.

No comments:

Post a Comment