KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Sunday, January 10, 2010

Timu ya Togo yashambuliwa Angola

Basi lililowabeba wachezaji wa timu ya taifa ya kandanda ya Togo limeshambuliwa muda mfupi baada ya kuvuka mpaka na kuingia nchini Angola, wakati likitokea kambi moja iliyopo Congo-Brazzaville, ambako timu ilikuwa ikifanya mazoezi.
Dereva wa basi aliuwawa na watu wengine kadhaa walijeruhiwa, wakiwemo wachezaji wawili.

Wachezaji waliojeruhiwa ni mlinzi Serge Akakpo aliyepata majeraha mabaya, pamoja na mlinda mlango wa akiba Kodjovi Obilale.

Togo ni miongoni mataifa yanayoshiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika inayofanyika nchini Angola, na itaamua leo ikiwa itaendelea na michuano hiyo.

Kundi moja la waasi wanaotaka kujitenga katika jimbo la Cabinda nchini Angola lilidai kuhusika na shambulizi hilo.

No comments:

Post a Comment