KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, November 9, 2009

Terry aizamisha Manchester United


Bao pekee la John Terry limeisogeza mbele Chelsea kwa pointi tano katika Ligi Kuu ya soka ya England na pia limeiteteresha Manchester United kutetea taji lake.
Nahodha huyo wa Chelsea aliunganisha kwa kichwa mpira wa adhabu ya moja kwa moja dakika za mwisho mwisho na kuifanya timu yake kupata ushindi wa 10 mfululizo katika uwanja wa nyumbani.Wayne Rooney mara mbili alikosa nafasi nzuri za kupata mabao, lakini bahati haikuwa upande wao mabingwa hao watetezi.

Wakati timu hiyo ya Sir Alex Ferguson ikiwa nyuma kwa pointi tano dhidi ya wapinzani wao hao wa London, Manchester United ni lazima wafanye kazi ya ziada kuipiku Chelsea ambao wanaonekana wamedhamiria kuwa mabingwa msimu huu.

No comments:

Post a Comment