KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Monday, November 9, 2009

Mputu tayari kucheza soka Ulaya

Nahodha wa klabu ya soka ya TP Mazembe Tresor Mputu Mabi amesema kwa sasa yupo tayari kuchezea klabu moja kubwa katika ligi ya Ulaya.
Mputu aliiongoza klabu yake hiyo ya DR Congo kunyakua ubingwa wa vilabu barani Afrika siku ya Jumamosi walipoilaza Heartland ya Nigeria.

Mchezaji huyo wa kiungo ni mchezaji hodari na pia ndiye anayelipwa vizuri barani Afrika.


Mputu amesema"Niliahidi timu hiyo sitaondoka katika klabu yangu kabla sijashinda kombe na kwa vile nimefanikiwa katika hilo nipo tayari".

Miaka miwili iliyopita Mputu alihusishwa na vilabu vikubwa barani Ulaya, lakini alichagua kubakia na klabu yake ya Mazembe hadi sasa.

No comments:

Post a Comment