KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, November 9, 2009

TP Mazembe mabingwa wa soka Afrika


TP Mazembe ya DR Congo imeilaza Heartland ya Nigeria bao 1-0 mjini Lubumbashi na kuweza kunyakua ubingwa wa ligi ya vilabu barani Afrika.
Katika mchezo wa awali wiki moja iliyopita Mazembe walifungwa mabao 2-1 ugenini na hivyo kuweza kushinda taji hilo kwa goli la ugenini.


Lakini hata hivyo ulikuwa ni mchezo mkali ulioshuhudiwa na mashabiki 35,000 mjini Lubumbashi ambapo Mazembe imezoa zawadi ya kikitita cha fedha dola milioni 1.5.

Mazembe waliwahi kushinda ubingwa wa vilabu vya Afrika mwaka 1967 na 1968 na mwaka huu walijiandaa kwa kutumia dola milioni 5 kujaribu kunyakua kombe hilo lenye hadhi kubwa barani Afrika.

Sehemu ya fedha hizo zilitumika kumuajiri kocha Mfaransa mwenye umri wa miaka 59 Diego Garzitto na utabiri wake kwamba mashabiki wa Congo wataondoka uwanja wa Kenya kwa mbwembwe umekuwa sahihi.

No comments:

Post a Comment