KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, November 9, 2009

Bent aitwa timu ya taifa ya England


Mshambuliaji wa timu ya soka ya Sunderland Darren Bent ametajwa katika orodha ya wachezaji wa kikosi cha England kitakachopambana na Brazil tarehe 14 Novemba katika mchezo wa kirafiki.
Mlinzi wa Aston Villa Stephen Warnock na kiungo wa Tottenham Tom Huddlestone nao pia wameitwa katika kikosi hicho cha Fabio Capello.

Mchezo huo utakaofanyika Qatar utakuwa wa mwisho kabla Capello hajataja kikosi chake cha awali kwa ajili ya kuiwakilisha England katika Kombe la Dunia.

Bent, ambaye hadi sasa ameshafunga mabao manane katika Ligi Kuu ya England anatarajiwa kung'ara kutokana na kukosekana kwa Emile Heskey ambaye ni majeruhi.

No comments:

Post a Comment