KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, November 4, 2009

Mafuriko yakumba kambi ya Daadab


Mafuriko yakumba kambi ya Daadab

Kambi kubwa zaidi nchini Kenya inayowahifadhi wakimbizi zaidi ya laki 2 kutoka Somalia, kaskazini mashariki mwa nchi imekumbwa na mafuriko baada ya mvua kubwa kunyesha.


Mafuriko yametokea katika kambi ya Daadab, baada ya mvua kuendelea kunyesha kwa zaidi ya wiki moja na sasa Inaarifiwa mojawapo ya kambi zinazowahifadhi wakimbizi hao ya IFO imesombwa na maji.

Wengi wamelazimika kuondoka kwenda maeneo salama huku mvua zaidi zikiendelea kunyesha.

Hali hii imetatiza shughuli za usafiri na upelekwaji wa chakula na mahitaji mengine kwa wakimbizi hao. Hata hivyo kufikia sasa hakuna ripoti za vifo

No comments:

Post a Comment