KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, November 4, 2009

Benki za Nigeria zawekewa sheria kali

Benki kuu ya Nigeria imeiamuru sekta ya benki nchini humo kuripoti utoaji na uingizaji fedha zenye kutia shaka kwa watu wanaohusika na siasa.
Hatua hiyo ni sehemu ya marekebisho yanayofanywa na gavana wa benki kuu Lamido Sanusi katika hatua za kusitisha ufisadi.

Bw Sanusi amewafukuza kazi wakuu wa benki tano na kuwashitaki kwa makosa ya udanganyifu wakurugenzi wa benki kadhaa.

Taratibu kama hizo ni kawaida katika maeneo mengine duniani tangu mashambulio ya kigaidi yalipotokea nchini Marekani tarehe 11 Septemba 2001.

No comments:

Post a Comment