KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Wednesday, November 4, 2009

Huenda McCarthy akauzwa Januari


Meneja wa Blackburn Rovers Sam Allardyce amesema inawezekana mshambuliaji Benni McCarthy akaondoka katika klabu hiyo wakati wa usajili mdogo mwezi wa Januari.

McCarthy mchezaji wa kimataifa wa Afrika Kusini mwenye umri wa miaka 31, inaarifiwa anajiandaa kuondoka Ewood Park mwaka mpya ujao wa 2010.

Allardyce ameiambia BBC kitengo cha michezo "Kwa umri alionao nafahamu anahitaji kucheza kikosi cha kwanza, lakini kwa wakati huu hawezi kufanya hivyo''.

Ameongeza"Iwapo anahitaji kupata fursa hiyo kwengine nitamuelewa."

McCarthy hajaanza kucheza tangu mwanzo katika mechi za Ligi Kuu ya soka ya England tangu Blackburn ilipofungwa mabao 2-0 na Manchester City katika ufunguzi wa msimu wa ligi hiyo.

No comments:

Post a Comment