KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Wednesday, November 4, 2009

Ancelotti avutiwa na kiwango cha Drogba


Meneja wa Chelsea Carlo Ancelotti amesema hatombadili Didier Drogba na mshambuliaji mwengine baada ya kupachika mabao mawili ya sare ya 2-2 na Atletico Madrid.
Drogba, aliyerejea baada ya kutumikia adhabu ya kutocheza michezo mitatu ya Uefa, amefikisha mabao 12 kwa msimu huu, huku Chelsea ikifanikiwa kuingia hatua ya mtoano ya timu 16 ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya.

"Nataka kuendelea kuwa naye na sitaki kumbadilisha na mshambuliaji mwengine yeyote'', amesema meneja wa Chelsea Ancelotti.

"Drogba yupo katika kiwango cha juu, nina furaha sana. Natumai ataendelea zaidi," ameongeza Ancelotti.

No comments:

Post a Comment