
Mlinzi wa Arsenal Gael Clichy hatocheza kwa wiki kadha baada ya kupata maumivu ya mgongo.
Clichy anayechezea nafasi ya ulinzi wa kushoto, alicheza siku ya Jumamosi ambapo Arsenal iliilaza Tottenham mabao 3-0, anatarajiwa kufanyiwa uchunguzi.

Kieran Gibbs atachukua nafasi yake katika mechi ya Jumatano ya ligi ya mabingwa wa Ulaya watakapochuana na AZ Alkmaar.

No comments:
Post a Comment