KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, November 9, 2009

Chavez aitisha kijeshi Colombia
Rais wa Venezuela Hugo Chavez ameyataka majeshi ya nchi yake kujiandaa kwa vita na Colombia kutokana na hali ya kidiplomasia na eneo la mpakani kutokuwa shwari.

Amesema njia bora zaidi ya kuepuka vita ni kujiandaa navyo. Ikijibu vitisho hivyo, Colombia imesema itaomba msaada kutoka Umoja wa Mataifa.

Venezuela imeshutumu kuongezeka hali ya wasiwasi na jirani yake kutokana na kuwepo uhusiano wa karibu baina ya Colombia na Marekani.

Colombia imesema majeshi ya Marekani yapo nchini mwake kwa ajili ya kupambana na waasi na wafanya biashara ya dawa za kulevya tu.

Bw Chavez pia amewaamuru wanajeshi 15,000 kuelekea mpakani kutokana na kuongezeka vurugu za wapiganaji wa Colombia.

No comments:

Post a Comment