KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, November 9, 2009

Mafuriko yaangamiza wengi El Salvador


Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchi hiyo Humberto Centeno amesema serikali imetangaza hali ya hatari katika mikoa mitano iliyoathirika vibaya na mafuriko hayo.
Serikali ya El Salvador imesema takriban watu 91 wameuawa nchini humo kutokana na mafuruko kufuatia mvua kubwa zilizonyesha.

Bw Centeno amesema mji mkuu San Salvador na mkoa wa kati San Vicente ndio iliyoathirika sana.


Mwandishi wa habari Juan Carlos Barahona ameiambia BBC, mkoa wa San Vicente kwa sehemu kubwa umepoteza mawasiliano na maeneo mengine kutokana na maporomoko ya ardhi na madaraja yaliyokatika.


Bw Barahona, anayeandikia gazeti la El Salvador daily La Prensa Grafica, amezidi kuifahamisha BBC, maeneo mengine yaliyoathirika vibaya ni La Libertad, La Paz na Cuscatlan.

Bw Centeno amesema watu 60 bado hawajulikani walipo na wengine 7,000 zaidi wamehifadhiwa.

No comments:

Post a Comment