KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Monday, November 9, 2009

Bashir akatisha ziara yake Uturuki


Rais wa Sudan Omar al-Bashir, anayeshtakiwa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, hatohudhuria mkutano wa nchi za Kiislamu mjini Istanbul.
Serikali ya Uturuki awali iliukubali ushiriki wa Rais Bashir katika mkutano huo na ikasema haitamkamata.


Lakini Umoja wa Ulaya ambapo Uturuki inadhamiria kujiunga nao, ilitaka mwaliko wa Bashir ufutwe.

Shirika la habari la Sudan, Suna limesema ''mambo muhimu yamemfanya Bw Bashir abakie Sudan.

Bw Bashirm alikuwa Misri siku ya Jumapili akihudhuria mkutano baina ya China na mataifa ya Afrika.

Alitazamiwa kuwasili Istanbul Jumatatu hii kuhudhuria mkutano wa nchi za Kiislamu(OIC).

No comments:

Post a Comment