KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Monday, October 5, 2009

Wapiganaji wa Nigeria wajisalimisha


Ahadi ya pesa na mafunzo ilitosha kuwashawishi wafuasi wa kundi moja kuu la waasi katika jimbo la Niger Delta kusalimisha silaha zao kufuatia msamaha uliotolewa na serikali.
Hatua za kujisalimisha ziliongozwa na kinara wa moja wa makundi hayo Government Tompolo ambaye aliridhika na ahadi za serikali kwa wapiganaji wake.

Hapo Jumamosi, makamanda wengine wawili kutoka eneo la mashariki mwa jimbo hilo walisalimisha silaha zao.

Kwa miaka mingi makundi ya waasi yamekuwa yakiendesha hujuma za kila aina na kuyashambulia makampuni ya mafuta kwenye jimbo hilo.

Kumekuwa na visa vingi vya utekeji nyara na makundi hayo kudai pesa za uokozi.

Lakini katika hatua ya kumaliza uhasama huo, serikali iliahidi kutowaandama wapiganaji hao, itawasamehe na kuwalipa pesa pamoja ikiwa ni pamoja kuwapa mafunzo.

Mamia ya watu walijitokeza kushuhudia sherehe hiyo ya kusalimisha silaha huku wakionyesha furaha kwamba hatimaye amani imepatikana katika jimbo hilo lenye utajiri mkubwa wa mafuta.

No comments:

Post a Comment