KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Tuesday, September 29, 2009
USICHO KIJUWA UNAHITAJI KUKIFAHAMU
USICHOKIJUWA KIPO NDANI YA GIZA LA NAFSI YAKO. HAKUNA JAMBO GUMU KATIKA MAISHA KAMA KUTEMBEA NDANI YA MSINGI WA GIZA NA UKUTA WA UPOFU. WATU WENGI WENYE MACHO TIMAMU, TUNAJIFUNZA MAMBO MENGI KUPITIA MIONO YA AINA MBALIMBALI, LAKINI KUNA MATENDO YENYE MAFICHO YA FAHAMU. LICHA YAKUWA BINADAMU, ANAMACHO YANAYOMUEZESHA KUONA VIZURI BILA HATA KUVAA MAWANI, LAKINI MARANYINGINE, BINAADAMU, TUNAJIKUTA TUKISHINDWA KUJUWA AU KUELEWA NI NINI MAANA YATENDO HUSIKA. KWA UPANDE MWINGINE TWAWEZA KUJIULIZA KWA NI NINI TUSIELEWE JAMBO FULANI, PINDI TUNA MACHO YENYE KUONA VIZURI!!!??
UKWELI WA MAMBO YOTE UNATOKANA NA ELIMU (UFAHAMU) YA NAFSI HUSIKA JUU YAJAMBO HUSIKA. MARANYINGINE WATU WANAJIULIZA KUHUSU NI NINI MAANA YA SWALI ! LAKINI JIBULAKE NI KWAMBA SWALI NI MFUMO AMBAO NAFSI YA MTU, INAUTUMIA ILI IWEZE KUPATA UFAHAMU (ELIMU YA UMUHIMU, UTENDAJI, FAIDA NA HASARA) JUU YA JAMBO (KIFAA KAMA GARI, MATENDO YA KIUMBE KAMA WANYAMA, NDEGE, SAMAKI, WADUDU, KUBADILIKA KWA HALI YA HEWA, RANGI, MAUMBILE YA WATU AU VIUMBE WENGINE, MASHINE, KUSOMA ,KUANDIKA………N.K) FULANI.
IKIWA NAFSI YA MTU HAIJUI KITU FULANI NA UMUHIMU WAKE NA FAIDA YAKE NA HASARA YAKE, KWA KWELI NAFSI HUSIKA ITAJIKUTA KATIKA HALI TETE YA KUTAFAKARI NA KUTAMANI KUJUWA MENGI KUHUSU KIUMBE AU KITU (MTU, WANYAMA, NDEGE, WADUDU, SAMAKI, SAFARI YA MWEZI NA JUWA….N.K)FULANI.
IKIWA KILA BINAADAMU ANGEWEZA KUWA MAKINI KATIKA KUTAFAKARI NA KUJUWA UMUHIMU, FAIDA NA HASARA YA JAMBO (NDOA, URAFIKI, WIZI, RUSHWA, UFISADI, LAWAMA, CHUKI, UPENDO, MSAADA…..N.K), BASI KILA JAMBO LINGEWEZA KUWA NA UANGALIFU MAISHANI MWA KILA BINAADAMU. KWASABABU LAWAMA, FITINA, UZINZI, CHIKI, LAANA, DHANA, MAUWAJI, MATUSI, UBAKAJI, USENGENYAJI, DHULMA, RIBA, INGEPUNGUA BAINA YA FAMILIA, KOO, NDOA, UCHUMBA, NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI, MFUMO WA KUTOA AU KUPOKEA DENI, IBADA, WEMA….N.K.
KWASASA DUNIA IMEJAA MALALAMIKO MENGI YA KULAUMIANA NA YACHUKI ZAIDI YA KUTENDEANA WEMA. KWA SASA MAUWAJI YA WATU YAMEKUWA KAMA MCHEZO WA KUIGIZA, VIFO VYA WATU WENGI WASIOKUWA NA HATIA KATIKA JINA LA UGAIDI, UDINI, ULEMAVU WA NGOZI, WIVU WA MAENDELEO, DEMOKARASI, UKABILA, KOO, MILIKI, BIASHARA…..NK, VIMEKUWA VINGI SANA NA BINADAMU WENGI TUMEISHA ZOELESHWA NA WANDALIZI WA MAUWAJI, KWAMBA KUWA AU KUUWAWA NIJAMBO LA KAWAIDA. KWENYE LUNINGA TUNAONA NA KUSIKIA.
MWALIMU WA MACHUNGU KWA SASA ANAONGOZA DUNIA KATIKA MFUMO WA UTANDAWAZI USIO KUWA NA MIPAKA KATIKA KULINDA NA KUTETEA HAKI ZA WANYONGE. SIKUSEMA KWAMBA HATUNA WATU WA BUSARA WENYE UWEZO WA KUKEMEA NA KULINDA UTUKUFU WA MWANADAMU, BALI WOTE WALIOWENYE BUSARA, WAMETINGWA NA UHABA WA ELIMU YA KISAYANSI NA KITEKNOROJIA, ILI WAWEZE KUKABILIANA NA HALI KUBWA INAYOANGAMIZA JAMII. NAWALE WENYE KUJITOKEZA NA KULINDA AU KUTETEA MASLAHI YA JAMII AU KOO AU FAMILIA ZAO HUITWA KUWA NI WENYE KUKOSESHA UHURU WATU KUFANYA MAMBO YAO. HAKUNA MTU MWENYE UWEZO WA KUONGOZA NAFSI YA MTU MWINGINE KATIKA HALI YENYEMSINGI WA MARIDHIANO, BALI KINACHOHITAJIKA NI USTARABU NA KUWA NA FAHAMU (ELIMU) YENYE MSINGI WA UTAMBUZI JUU YA JAMBO BAYA NA ZURI, ILI KILA BINAADAMU AWEZE KUISHI KATIKA HALI YA MARIDHIANO, BAINA YA KOO, DINI, MAKABILA, RANGI NA TAMADUNI MBALIMBALI.
31.08.09
KILA JAMBO MAISHANI LINAWEZEKANA KWA KUELEWANA KATIKA MSINGI WA UPOLE NA WENYE ELIMU (UFAHAMU) JUU YA KILA JAMBO LINALOTENDEKA. IKIWA LINA KASORO BASI KILA MTU MWENYE KIPINGAMIZI AWE HURU KATIKA MAONI NA KUTOA HOJA AU SWALI ILI AWEZESHWE KUPATA MSAADA WA KUELEWA UMUHIMU, FAIDA NA HASARA VYA JAMBO (KITENDO AU MANENO ) HUSIKA. NJIA HII ITAWEZA KUONDOA DHANA YA KUONA KWAMBA WATU WATU FULANI HAWANA USTARABU AU DINI FULANI NIYENYE CHUKI JUU YA DINI NYINE AU DINI FULANI HUTUMIA MABAVU KATIKA KUANGAMIZA WATU KATIKA JINA LAMU WAO, AU DINI FULANI IANGAMIZWE KATIKA JINA LAKUPIGWA VITA MAGAIDI. HII SIO NJIA SAHIHI, BALI ITAKUZA CHUKI BAINA YA WATU WENYE KUISHI BILA KUJALI DINI, KOO, RANGI……….N.K.
KUNA ELIMU MUHIMU NA LAZIMA KILA MTU MWENYE AKILI AJUWE KWAMBA KUFAHAMU KINACHOENDELEA DUNIANI, LAZIMA AWE MAKINI KATIKA MSINGI WA KUTAFAKARI UMUHIMU FAIDA NA HASARA YA KILA JAMBO LINALOSEMWA NA KUTENDWA DUNIANI.
KUNA TAFAUTI YA KULIPIZA KISASI NA DINI. IKIWA DINI FULANI MUONGOZO WAKE NI KUMJUWA MUNGU NA KUTENDA MAPENZI YA MUNGU, INAKUWAJE DINI HIO IWE NIYENYE KUAMRISHA WATU WAKE KUJILIPUA NA KUANGAMIA NA KUANGAMIZA WATU ?
KWA KWELI KUNA SIRI YENYE KUHITAJI UMUHIMU, FAIDA NA HASARA JUU YA DHANA HII. DINI NI MUONGOZO WA KUTENDA MEMA NA KUKATAZA MABAYA INAKUWAJE DINI IENDE KINYUME NA MAANDIKO YA MUNGU?
KULIPIZA KISASI KUNATOKANA NA KUSHINDWA KUVUMILIA KWA NAFSI HUSIKA. MWENYE KULIPIZA KISASI ANAWEZA KUKILIPIZA JUU YA YULE MUUWAJI, AU UKOO WAKE AU KABILA LAKE. NDIO MAANA KILA KUKICHA TUNASHUHUDIA VIFO VYA MASHAMBULIZI YA KIVITA NA KIDINI BAINA YA WAYAHUDI NA WARABU AU BAINA YA WANAJESHI WAJAMIVI WA NCHI ZA WARABU. YOTE HAYO YANATOKANA NA UPUNGUFU WA ELIMU JUU YA HASARA, FAIDA NA UMUHIMU WA VITA HUSIKA AU WASHAMBULIAJI NA WASHAMBULIWAJI.
NJIA HII IMEWEZA KUVURUGA UHSIANO MKUBWA WA MAPENZI BAINA YA DINI, KOO, MAKABILA, RANGI………………………..N.K.
MENGI YAMETOKANA NA THAMANI YA BINAADAMU KUPUNGUZWA NA UKOSEFU WA ELIMU YA KUTOSHA JUU YA UMUHIMU, FAIDA NA HASARA YA JAMBO (KUOA AU KUOLEWA, KUZAA AU KUTOZAA, MALEZI AU KUTOLEA, KUONGOZA AU KUONGOZWA, KUMILIKI AU KUTOMILIKI, KUABUDU AU KUTOABUDU, KUFANYA KAZI AU KUTOFANYA KAZI, KULAUMU AU KULAUMIWA, KUZINI AU KUZINIWA, KULEA AU KULELEWA, KUCHUKIA AU KUCHUKIWA, KUUWA AU KUULIWA, KUIBA AU KUIBIWA, KUJENGA AU UKOSEFU WA HIFADHI YA NAFSI, KULISHA AU KULISHWA, KUNYWESHWA AU KUNYWESHA………………………….N.K.
MAMBO HAYA NI MAMBO YENYE MALALAMIKO YA HALI YA JUU KABISA.
UKIANGALIA KATIKA FAMILIA NYINGI SANA ZA KIAFRIKA WENGI NI WABINAFSI NA HATUPENDI KUONA NDUGU, JAMA NA MARAFIKI WAKIFANIKISHA MAMBO YAO AU TUKIWAPA HONGERA KWAKAZI YAO YA KUJENGA TAIFA NA KUTOA AJIRA NA MISAADA KWA WENGI. BALI WENGI WETU HUWA NI WENYE KUTENGENEZA MAZINGIRA YA KUKATISHANA TAMAA ZA KIMAENDELEO NA MARANYINGINE TUKITENGENEZEANA MITEGO YA KUCHAFUANA KIVITENDO NA KIKAULI NA MARANYINGINE KUTAFUTIANA SABABU YA KUFILISIANA NA MARANYINGINE TUKIENDEANA KWA WAGANGA ILI TUHARIBIANE BIASHARA NA MARANYINGINE TUKIANZISHA VITIMBI VYENYE DHANA YA UDINI ILI TUGAWANYIKE KATIKA MATABAKA YA KIDINI NA UKABILA ILIMRADI FULANI AKOSE NA SI TUKOSE AU AFE AU AFIRISIKE KAZI HIYO TUIFANYE SISI. TABIA HII NITABIA YENYE KUTENDWA NA NYOYO ZENYE MSINGI WA GIZA NDANI YA NAFSI ZAKE. KWA SABABU IKIWA WEWE NI ISMAIL NA YULE NI ISMADO JUWA KWAMBA MWENYEZI MUNGU ALIMUUMBA KILA MTU NA RIZIKI YAKE.
IKIWA KILA BINAAADAMU ANA MFUMO WA SURA YAKE NA MSINGI WA MAONGEZI NA MATENDO YAKE, BASI FAHAMU YA KWAMBA SURA YA MTU PAMBO LAKE NI MATENDO YAKE NA MANENO YAKE. NA NDIO MAANA UNAWEZA KUMUONA MWANAMKE MZURI AU MWANAMME MZURI WA SURA, HANA HESHIMA WALA PESA MAISHANI MWAKE LAKINI UKAMUONA MWANAMKE MBAYA NA MWANAUME MBAYA WA SURA
(KILA NAFSI INA MTAZAMO WAKE WA KUCHAGUA SURA NZURI AU MBAYA), AKAWA NA UWEZO WA KUHESHIMIWA NA WATU NA KUMILI AU KUWA NACHEO KIKUBWA KABISA. MARANYINGI HESHIMA NA UZURI WA SURA NI VITU VIWILI TOFAUTI. KWASABABU UNAWEZA KUWA MZURI WA SURA AU UMBILE UKAPEWA KAZI FULANI ( UMISI, KUKARIBISHA WAGENI HOTELINI AU KWENYE NDEGE, KWENYE MADUKA MAKUBWA AU KWENYE KASIRI LA MFALME), NA UKAKOSA KUPEWA HEMA NA WATU AU NA WALE AMBAO WATAKUPA HESHIMA WANAWEZA KUKUPA HESHIMA YA KINAFIKI, ILI USIWANYIME HAKI YAO AU WAKITEGEMEA KUPATA CHOCHOTE KWAKO.
HII NI HESHIMA AMBAYO NIYA KUPANDIKIZWA KATIKA MAZINGIRA YAKUPEWA NAFASI KWA AKILI YA UBORA WA SURA AU UMBILE. UGUMU AU UTATA WA WAKUPATA HESHIMA UNATOKANA NA UKOSEFU MA UFAHAMU WA MATUMIZI BORA YA MANENO NA MATENDO YA NAFSI.
MZUNGUUKO WA MAISHA UNAAMBATANA SIKU ZOTE NA UFAHAMU (ELIMU) BORA WA MATUMIZI MAZURI YA MUONO NA USIKIVU. USIKIVU UNAPATIKANA AU UNAINGIZWA NDANI YA NAFSI NA VIFAA MALUMU AMBAVYO NI MASIKIO. UNAPOSIKIA SAUTI AU NENO NGENI, LAZIMA UKIWA NA AKILI TIMAMU, UWE NA SHAUKU LA KUJUWA UMUHIMU, FAIDA AU HASARA YAKE. NJIA HII ITAKUPA NAFASI BORA YA KUJILINDA AU KUTUMIA KWA MAKUSUDI MFUMO BORA WA MAJIBU YENYE MFUMO WA MATENDO NA MANENO BORA. KINYUME CHAKE, UTAKUWA NI MWENYE KULAUMU AU KULAUMIWA BILA KUJUWA KWAMBA TATIZO NI NINI. KUMBE TATIZO NI KULE KUELEWA KWMBA USICHO KIJUWA UNATAKIWA KUKIJUWA ILI UEPUKANE NA VITIMBWI VYAKE MAPEMA.
MUANDISHI NI : ISMAIL MUSA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment