KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Monday, October 26, 2009

Shambulio baya zaidi la mabomu Iraq


Maafisa wa polisi mjini Baghdad, wamesem milipuko ya mabomu kutoka magari mawili ya watu waliojitoa mhanga yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 130, na kujeruhi zaidi ya wengine 500.
Hayo yamekuwa ndio mashambulio mabaya zaidi kuwahi kutokea nchini Iraq tangu mwaka 2007.

Milipuko hiyo ya mabomu ilifanyika moja baada ya jingine, na kuharibu majumba ya wizara ya afya, na jumba lingine lenye afisi katikati ya mjini Baghdad.

Wafanyikazi wa uokozi bado wanajaribu kuinua vifusi katika juhudi za kuwatafuta watu zaidi walionusurika.

No comments:

Post a Comment