KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, October 26, 2009

Pakistan yateka mji muhimu wa Taliban


Vikosi vya Pakistani vimeuteka mji mkuu uliokua mikononi mwa Wataliban wa Kotkai huko Waziristan ya kusini.
Mji huo ulitekwa na vikosi kufuatia siku kadhaa za kuushambulia kwa makombora. Kwa mujibu wa maofisa wa jeshi a Pakistan askari watatu na wapiganaji wanne wa Taliban imearifiwa waliuawa katika mapigano ya usiku.

Mji wa Kotkai, ndiko ambako kiongozi wa ngazi ya juu wa Taliban Hakimullah Mehsud, umeshuhudia mapigano makali tangu Pakistan ianze kampeni yake ya kushambulia Waziristan ya kusini wik iliyopita.


Wandishi habari wamekatazwa kufika katika eneo hilo wala hawawezi kuthibitisha taarifa zinazojitokea huko.

Hadi sasa takriban raia 100,000 wamekimbia medani ya vita, kwa mujibu wa jeshi la Pakistan.

Iliarifiwa mapema wii hii Vikosi vya Pakistan vikiwa na makombora, helikopta pamoja na ndege za kivita viliuteka mji wa Kotkai kwa mda kabla ya Taliban kurudi kwa nguvu wakiua askari saba wa Pakistan kuvunja vizuzi na kuurejesha mikononi mwao wiki hii.

No comments:

Post a Comment