KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Monday, October 26, 2009

Ofisi za MDC zavamiwa na polisi


Polisi nchini Zimbabwe wamevamia nyumba inayomilikiwa na chama cha Waziri Mkuu Morgan Tsvangirai cha MDC kwa maelezo walikuwa wakisaka silaha.
Tendai Biti, Katibu Mkuu wa MDC amesema zaidi ya askari polisi 50 walipekua kila ofisi siku ya Ijumaa jioni.

Bwana Biti amesema polisi walichukua vitu muhimu vya chama cha MDC kutoka katika chumba cha katibu mipango wa chama hicho, Morgan Komichi.

Wiki iliyopita Bw Tsvangirai alitangaza chama cha MDC kitasusia shughuli zote za serikali ya umoja.

Chama cha MDC kinamshutumu Rais Robert Mugabe kwa kuwakandamiza wapinzani wake wa kisiasa na ameshindwa kutekeleza makubaliano ya serikali ya umoja.

No comments:

Post a Comment