KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Monday, October 26, 2009

Karadzick asusia kuanza kwa kesi


Kiongozi wa zamani wa Waserb wa Bosnia Serb Radovan Karadzic ameshindwa kufika mahakamani ambapo anakabiliwa na mashtaka 11 yakiwemo mauaji, uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu.
Bw Karadzic amekanusha mashtaka yanayomkabili ambayo yanahusishwa na vita vya Bosnia vya miaka ya 1990.

Jaji aliahirisha kesi hiyo kwa siku moja, huku upande wa mashtaka ukitarajiwa kutoa maelezo siku ya Jumanne.

Jaji amemtaka Bw Mr Karadzic, ambaye amesema anahitaji muda zaidi wa kuandaa utetezi wake, kufika mahakamani ili kuwezesha kesi kusikilizwa.

Bw Karadzic, mwenye umri wa miaka 64, alipelekwa katika mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ya The Hague mwaka jana baada ya kujificha kwa muda wa miaka 13.

No comments:

Post a Comment