KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, October 26, 2009

Benitez asifu uwezo wa Torres


Meneja Liverpool Rafael Benitez amemsifu Fernando Torres baada ya kuwa mwiba kwa ushindi wao wa mabao 2-0 dhidi ya Manchester United.
Torres amekuwa akisumbuliwa na maumivu ya nyonga, lakini aliweza kufunga bao la kuongoza dhidi ya Manchester United baada ya Benitez kuamua kumchezesha tangu mwanzo.

Benitez amesema"Unaweza kuona hakuwa imara kwa asilimia 100, lakini Fernando akiwa imara asilimia 80 tu anaweza kuleta mabadiliko".

Torres aliunganishiwa pasi na Yossi Benayoun na akaweza kumshinda mlinzi Rio Ferdinand kabla ya kuachia shuti kali karibu na lango.

Alitolewa nje katika dakika ya 80 kutokana na Benitez kutotaka kubahatisha kuendelea kumchezesha ili asije kujeruhiwa na aweze kucheza michezo ijayo

No comments:

Post a Comment