KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, October 26, 2009

Man United yapata kipigo


Klabu ya Liverpool ilimaliza mkosi wake wa matokeo mabaya kuwahi kuonekana tangu mwaka 1987, na pia kuondoa shinikizo kutoka kwa kocha wake Rafael Benitez kwa njia ya kipekee kwa kuizabua Manchester United.


Mshambuliaji Fernando Torres alionesha umahiri wa kustaajabisha kwa kuandika bao la kwanza katika dakika ya 65, baada ya kumzidi beki Rio Ferdinand na kuachia mkwaju mkali ambao kipa Edwin van der sar hakuweza hata kuuona ulipopita.

Liverpool ilipata ushindi wa mabao mawili kwa sifuri na kufufua mbio zake za kuwania ubingwa wa ligi kuu ya England.

No comments:

Post a Comment