KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Monday, October 26, 2009

Chelsea waongoza ligi ya Premier


Chelsea wamekwea ulingo wa ligi kuu ya England baada ya kuicharaza Blackburn Rovers kwa mabao 5 kwa 0.
Ushindi huu wa Chelsea umeiwezesha kuikiuka Manchester United ambayo inachuana na Liverpool katika pambano kali la Jumapili.

Katika michuano mingine ya siku ya Jumamosi Stoke City ilitamba ugenini na kuigutua Tottenham Hotspurs 1-0.

Aston Villa ikatoka sare 1-1 na Wolvehampton Wanderers.

Birmingham ikaichapa Sunderland 2-1.

Bunley ikalala nyumbani 3-1 dhidi ya Wigan na Hull ikatoka sare bila kufungana na Portsmouth.

Chelsea ina ponti 24 baada ya mechi kumi.

No comments:

Post a Comment