KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, October 27, 2009

Maharamia wateka mashua ya anasa


Maharamia wateka mashua ya anasa

Msako unaendelea kuitafuta mashua ya anasa yenye Waingereza wawili mtu na mkewe, wanaoaminika wametekwa na maharamia wa Kisomali karibu na Seychelles.
Paul na Rachel Chandler, kutoka Tunbridge Wells, Kent, walikuwa wakielekea Tanzania kwa kutumia mashua yao ya anasa iitwayo Lynn Rival.

Siku ya Ijumaa walitoa ishara ya kukabiliwa na hatari, lakini tangu wakati huo hawajasikika tena.

Mwandishi wa BBC wa masuala ya usalama Frank Gardner, amesema kwa taarifa alizonazo anaamini wamepelekwa Somalia.

Amesema inaaminika Waingereza hao pamoja na mashua yao wamepelekwa katika bandari ya Haradheere.

No comments:

Post a Comment