KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Tuesday, October 27, 2009

Marekani yamzuia afisa wa Kenya kusafiri


Marekani yamzuia afisa wa Kenya kusafiri

Marekani imemuwekea kikwazo cha kusafiri afisa mmoja wa ngazi ya juu nchini Kenya, kwa kuzuia juhudi za kutokomeza ufisadi nchini humo.
Mkuu wa idara ya mambo ya nje ya Marekani inayoshughulikia Afrika Johnnie Carson amesema pia anatafakari kuweka kikwazo kama hicho kwa maafisa wengine watatu, ingawa amekataa kutaja majina yao.

Kenya ilikubali kufanya mabadiliko, baada ya watu 1,300 kufa baada ya ghasia za baada ya uchaguzi mwaka jana.

Hata hivyo Marekani inaamini kuwa baadhi ya maafisa wamekuwa wakizuia kwa makusudi, hatua za mabadiliko hayo.

No comments:

Post a Comment