KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, October 5, 2009

Kwa hivi sasa rais wa sasa Hamid Karzai rasmi ametangazwa kuwa anaendelea kuongoza mbele ya mgombea wa karibu yake Abdullah Abdullah



Kwa hivi sasa rais wa sasa Hamid Karzai rasmi ametangazwa kuwa anaendelea kuongoza mbele ya mgombea wa karibu yake Abdullah Abdullah. Lakini pamoja na hayo kuna mapungufu mengi yaliyojitokeza katika uchaguzi huo. Taarifa ya Kai Küstner inasomwa studioni na Sekione Kitojo.
Kwa mara ya kwanza katika zoezi hilo la kuhesabu kura Hamid Karzai amefikia hatua ambayo hakuna mgombea mwingine anayeweza kuifikia ya zaidi ya asilimia 50. Iwapo hali hiyo itaendelea , rais huyo wa sasa tayari atakuwa amefanikiwa katika duru ya kwanza kupata ushindi. Kama tume huru ya uchaguzi inavyoeleza, Karzai hivi sasa ana asilimia 54 ya kura, na mgombea wa karibu Abdullah Abdullah anafuatia akiwa na zaidi ya asilimia 28. Wakati kiasi cha asilimia 90 ya kura zimekwisha hesabiwa.
Je hesabu hii ni halali kiasi gani, kwa kweli hadi sasa haifahamiki. kwa upande mwingine tume ya kusikiliza malalamiko, imeweka kando baadhi ya matokeo hayo. Kama anavyoelezea muangalizi wa uchaguzi huo ulioungwa mkono na umoja wa mataifa , ameueleza uchaguzi huo kuwa katika uchunguzi wao imeonekana ushahidi wa kutosha kuwa kulikuwa na udanganyifu. Alim Seddiqi msemaji wa umoja wa mataifa , amesema kuwa matatizo ya kutokufuata kanuni yalikuwa makubwa.
Tunaitaka tume ya uchaguzi ya Afghanistan pamoja na tume ya kusikiliza malalamiko kuongeza juhudi zao maradufu, ili kuhakikisha kuwa kuna juhudi kubwa katika kazi zao katika kila hatua. Hii ni pamoja na kuondoa kutoka katika matokeo ya mwisho hesabu ya masanduku ambayo yanadaiwa kuwa yalihusika katika udanganyifu. Uhalali wa uchaguzi huu ni muhimu sana kwa Afghanistan na washirika wake wa kimataifa.
Shutuma hizi za udanganyifu zinaelekezwa kwa upande wa Karzai. Taarifa zinasema kuwa katika jimbo moja la uchaguzi rais Karzai amepata asimilia 100 ya kura. Wagombea wengine wametoka mikono mitupu. Muda mfupi tu baada ya uchaguzi huo , taarifa zilieleza kuwa katika kituo kimoja cha uchaguzi masanduku ya kura yamegunduliwa yamejazwa kura bandia. Gazeti la New York Times limeeleza kuhusu mamia ya wapiga kura hewa, ambamo wapiga kura laki moja walijiandikisha na kumpigia kura Karzai, licha ya kuwa hakuna mtu aliyepiga kura katika eneo hilo. Katika jimbo anakotoka Karzai la Kandahar kwa mfano , matokeo yanaonyesha kuwa kulikuwa na wapiga kura 350,000, lakini wachunguzi wa mataifa ya magharibi wameona si zaidi ya watu 25,000 , ambao wamepiga kura katika jimbo la Kandahar.
Matokeo halali ya mwisho yatapatikana iwapo tuhuma hizo za udanganyifu zitapatiwa maelezo, na wachunguzi wa uchaguzi huo wanafikiria kuwa wiki kadha zitapita kabla ya kupata jibu.
Pamoja na hayo kuhusiana na jaribio la kupata maelezo ni pamoja umoja wa mataifa, NATO na serikali ya Afghanistan kuhusiana na shambulio lililoamriwa na jeshi la Ujerumani katika jimbo la Kunduz Ijumaa iliyopita. Katika maelezo yake jeshi linaloimarisha usalama nchini Afghanistan limesema siku ya Jumanne, kuwa matokeo ya uchunguzi wake yanatarajiwa baada ya wiki kadha. Hii ina maana pia kuwa uchunguzi unadhaniwa kuwa unaweza kuondolewa , kwasababu katika shambulio hilo pamoja na wapiganaji hata raia waliuwawa na wengine wamejeruhiwa.
Raia pia waliuwawa katika shambulio la hivi karibuni kabisa mjini Kabul jana Jumanne. Muuaji aliwalenga wazi wanajeshi kutoka nje, katika lango la kambi ya jeshi iliyoko katika uwanja wa ndege baada ya kuilipua gari aliyokuwa akiendesha. Taliban wanafahamika kwa mashambulio haya. Mkuu wa kikosi cha uhalifu katika jeshi la polisi mjini Kabul amesema kuwa watu watatu wameuwawa, na wengine sita wamejeruhiwa.
Mwandishi Kai Küstner / ZR / Kitojo, Sekione
Mhariri :Othman Miraji

No comments:

Post a Comment