KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, October 26, 2009

Kenya yasita kutoa vitambulisho


Maafisa wa serikali nchini Kenya wamesitisha shughuli ya kutoa vitambulisho katika mkoa wa Kaskazini-Mashariki, kufuatia madai kwamba baadhi ya wageni pia wamekuwa wakijiandikisha.
Mkuu wa mkoa Bw James Ole Seriani amewalaumu baadhi ya maafisa wa serikali kwa kuchukua hongo ili kuwapa wageni vitambulisho vya taifa hilo.

Kuna zaidi ya wakimbizi 300,000 kutoka Somalia wanaoishi katika mkoa huo.

Hata hivyo kuna watu wenye asili ya Kisomali ambao Kenya ni nchi yao halisi, na kama Wakenya, wanahitaji vitambulisho katika kufungua akaunti za benki, kutafuta kazi au hata kujiandikisha kujiunga na vyuo vikuu.

No comments:

Post a Comment