KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Monday, October 26, 2009

Nigeria yapona chupuchupu


Wenyeji na mabingwa watetezi Nigeria waponea chupuchupu na kutoka sare ya mabao 3 kwa 3 dhidi ya mabingwa wa Ulaya Ujerumani katika mechi yao ya ufunguzi ya michuano ya fainali za kombe la dunia la chipukizi wa chini ya umri wa miaka 17.
Ujerumani iliongoza 2-0 katika nusu ya kwanza na kuongeza bao la 3 katika dakika ya 47.

Vijana wa Nigeria wakaanza kuzinduka katika dakika ya 53 na kurudisha mabao 3 katika kipindi cha dakika saba.,baada ya mchezaji Robert Labus kuonyeshwa kadi nyekundu .

Katika michuano mengine Brazil iliishinda Japan kwa mabao 3 kwa 2. Nayo Argentina ikailaza Honduras 1-0.

No comments:

Post a Comment